Maalim Seif na Zitto Kabwe Watua Marekani..Tazama Picha Hapa


Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wamekutana Katika Mkutano Maalum wa Viongozi wa Kisiasa Ulimwenguni (International Leaders Forum) ambao unafanyika leo Asubuhi ‘Kwa Saa za Marekani’ Jijini Philadelphia.

Mkutano huo ulioandaliwa na asasi ya NDI ‘National Democratic Institute’, ni Sehemu ya matukio maalum kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention), Mkutano ambao utamthibitisha Bibi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais Kupitia Chama Hicho.

Zitto Kabwe Pamoja Na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim watakuwa Philadelphia mpaka Siku ya alhamis ambapo mkutano huo unategemewa kumuidhinisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais wa Marekani kupitia Chama Hicho.


Zitto Kabwe


Zitto Kabwe na Maalim Seif

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post