Utafiti: Kukaa na Kutazama TV Kwa Muda Mrefu Kunasababisha Kifo

Utafiti huu umeripotiwa na BBC ambapo imeelezwa kuwa umefanywa na wanasayansi wa Japan ambapo umethibitisha kwamba kukaa kwa muda mrefu na kutazama vipindi vya televisheni kwa saa nyingi kunahatarisha afya kwani kunahusishwa na maradhi yanayosababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.

Watafiti hao wamesema hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile mapafu husababisha vifo.



Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku. Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.

Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, hatari ya kupata ugonjwa wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40.

Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa muda wa chini ya saa 3.



Aidha watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527