Bohari la Matairi Lateketea Kwa Moto Jijini Dar es salaam



Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia matairi pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Bohari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego


Kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo







Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea

Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo

Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo






Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari

Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua

Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527