Picha 16!! Stand United Yafungua Pazia la Usajili..Tayari Wachezaji Watano Leo Wamelamba Mikataba,Wamo Wawili Kutoka Toto Africans

Kamati ya usajili ya klabu ya Stand United Fc ya mkoani Shinyanga imeanza zoezi la usajili kwa kusajili wachezaji watano hii leo huku wachezaji wawili wakitokea timu ya soka ya Toto Africans ya jijini Mwanza.


Akitambulisha wachezaji hao mbele ya waandishi wa habari mjini Shinyanga,mwenyekiti wa klabu hiyo Dr. Ellyson Maeja amesema uongozi wa klabu hiyo umejipanga kuhakikisha inafanya usajili wenye tija ili kuifanya timu hiyo kuwa tishio katika ligi kuu Vodacom Tanzania bara msimu ujao.

Dr.Maeja amewataja wachezaji waliowasajili kuwa ni Miraji Mussa Maka na Erick Muriro wote kutoka Toto Sports Club ya jijini Mwanza.

Wengine waliosajiliwa ni Adam Paul Salamba,John Biseko Mutobesha na Charles Ibreck wote kutoka Bulyanhulu Sports Club wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti huyo wa Stand United Dr. Maeja amesema bado wanaendelea na usajili na kwamba lengo lao ni kusajili kikosi cha wachezaji 25.

“Bado tunaendelea na zoezi la usajili na kesho Ijumaa Julai 01,2016 tunatarajia kusajili wachezaji wengine watatu kutoka mgodi wa dhahabu wa North Mara ili kukamilisha idadi ya wachezaji sita kutoka mgodi wa Bulyanhulu na North Mara”,amesema Dr.Maeja.

Dr. Maeja amewaondoa hofu mashabiki wa soka mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla kuwa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia bado ina dhamini klabu hiyo na mkataba wao wa miaka miwili bado haujaisha.

Wakizungumza baada ya kusaini mkataba tayari kuanza kuichezea Stand United wachezaji hao waliosajiliwa leo wamesema lengo la kujiunga na klabu hiyo ni kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo ili klabu hiyo ifanye vizuri katika michezo mbalimbali.


Kushoto ni Erick Mriro Mchezaji kutoka Toto Africans Club akisaini mkataba kujiunga na klabu ya Stand United,kulia ni mwenyekiti wa Stand United ,Dr.Ellyson Maeja

Kushoto ni katibu mkuu wa timu ya Bulyanhulu FC Dickson Lusingi ambaye ndiyo msimamizi wa timu hiyo iliyoko daraja la pili akizungumza wakati wa kuwakabidhi wachezaji wake watatu walioamua kujiunga na Stand United
Kulia ni Dr. Maeja akiwatoa maelezo kabla ya kumkabidhi mkataba mchezaji Paul Salamba kutoka Bulyanhulu Fc
Adam Paul Salamba (kushoto) akipitia mkataba kabla ya kuusaini

Dr. Maeja akimpa bahasha Adam Paul Salamba

John Biseko Mutobesha akutoka Bulyanhulu Fc akisaini mkataba kuichezea Stand United

Mutobesha akisaini mkataba

Golikipa kutoka Bulyanhulu Fc Charles Ibreck Minza akisaini mkataba kujiunga na Stand United

Wachezaji wapya wa Stand United wakiwa katika picha ya pamoja

Mwenyekiti wa Stand United Dr. Maeja akifurahia usajili mpya

Dr. Maeja akizungumza baada zoezi la usajili kukamilika

Adam Paul Salamba akizungumza baada ya kusaini mkataba

John Biseko Mtobesha akizungumza baada ya zoezi la usajili kumalizika

Erick Mriro akizungumza baada ya zoezi la usajili kumalizika
Kushoto ni katibu mkuu wa Bulyanhulu FC bwana Dickson Lusingi akifurahia jambo na katibu msaidizi wa Stand United bwana Emmanuel Kaombwe baada ya kuwakabidhi vijana wake watatu tayari kuanza kuitumikia Stand United -Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post