Baada ya Lipumba Kuunyemelea Tena Uenyekiti wa CUF..Viongozi wa CUF Watangaza Msimamo Wao


CHAMA cha wananchi CUF kimesema mkutano mkuu wa taifa ambao unategemewa kumpata Mwenyekiti wa chama hicho, upo pale pale, na kuweka msimamo kuhusu Ibrahimu Lipuma kuwa kama anataka kurejea katika nafasi yake achukue fomu.


Tamko hilo ni kufuatia sintofahamu kwa wanachama wa chama hicho kuwa huenda mkutano mkuu usiwepo kutokana na ujio wa ghafla wa Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa Mwenyekiti wa chama ambaye alijihudhuru cheo hicho.


Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho amesema tayari fomu za ugombea zimeshapelekwa katika ofisi ya wilaya tayari kwa kujazwa.


“Kuanzia 1 Julai washiriki katika ngazi ya Mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa chama pamoja na Makamu mwenyekiti wachama hicho na wataanza kuchukua fomu hadi Julai 20,” amesema.


Amesema, 21 Agosti baada ya zoezi la ujazaji fomu kukamilika, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Kitaifa watakaa kuchagua viongozi hao katika ukumbi wa Land Mark Ubungo Jijini Dar es Salaam.


Lipumba alijihudhuru katika kipindi cha uchaguzi Mkuu 25 Oktoba kutokana na sababu aliyoitoa kuwa ni uwepo wa aliyekua Mgombea urais, Edward Lowassa kuwa alihamia kwenye chama kwa kutofuata utaratibu.


Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema kutokana na katiba ya chama, Lipumba hatakiwi kurudi katika nafasi hiyo kwa kutengua kujiuzulu kwake isipokuwa kama anahitaji nafasi hiyo achukue fomu upya kugombea nafasi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Taifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post