WAZIRI NAPE AKERWA NA WATENDAJI WA SERIKALI KUNYANYASA WAANDISHI WA HABARI

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye amesema Serikali haitaendelea kuwavumilia baadhi ya watendaji wake wanaokwamisha uhuru wa vyombo vya habari kwa kuwakamata waandishi wanaochunguza ubadhirifu wa mali za umma ili kulinda maovu yao.
 
Msimamo huo wa Serikali umetolewa jijini Mwanza na Waziri Nape Nnauye wakati akizungumza na watendaji wa taasisi za umma zilizopo chini ya wizara yake,kufuatia tukio la kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Sahara Media Group wilaya ya Chato mkoani Geita Baraka Tizilamusomi, kulikofanywa na Jeshi la Polisi baada ya mwandishi kwenda kutibiwa katika hospitali ya wilaya hiyo Jumatano wiki hii.Serikali katika wilaya ya Chato imesambaza waraka kwenye taasisi zote za umma unaozuia waandishi wa habari kupata taarifa bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya,hali inayosababisha kuminya uhuru wa kupata habari ambao umetajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post