Utafiti : WATU WANENE NDIYO WENGI ZAIDI DUNIANI,WANAWAKE VINARA


Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani.

Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo cha Imperial cha London, wakiandika katika jarida la kimatibabu la Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene.

Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu.

Profesa Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna "mkurupuko wa unene".

Wanasayansi hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya kuendeshea baiskeli.

Wanazihimiza serikali kuchukua hatua za pamoja, hasa kuhusu bei ya vyakula.

Baada ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba idadi ya watu wanene duniani imeongezeka kutoka 105 milioni mwaka 1975 hadi 641 milioni mwaka 2014.

Idadi ya watu walio na uzani wa chini ya kuwango imeongezeka kutoka 330 milioni hadi 462 milioni katika kipindi hicho.

Viwango vya unene miongoni mwa wanaume kilipanda kutoka 3.2% mwaka 1975 hadi 10.8%, na miongoni mwa wanawake viwango vya unene vilipanda kutoka 6.4 % mwaka 1975 hadi 14.9%.

Hii ina maana kulikuwa na wanaume wanene 266 milioni na wanawake wanene 375 milioni mwaka 2014.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527