TCCL WAIOMBA SERIKALI KUWAMILIKISHA MKONGO WA MAWASILIANO WA TAIFAKAMPUNI ya Mawasiliano ya simu Tanzania TTCL imeiomba serikali kuwamilikisha mkongo wa mawasiliano wa Taifa ili kampuni hiyo waweze kuuendesha wao kutokana na uwezo walionao na mafundi na wataalamu wa kutosha.

Ombi hilo lilitolewa na meneja wa TTCL Mkoani Kigoma,Abdalah Lugage wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano wakati alipotembelea ofisi hizo.


Alisema shirika hilo linauwezo wa kusambaza mawasiliano katika ofisi zote na mpaka sasa wamefikia uwezo wa internet 4G ambayo inatumiwa na ofisi zote za serikali na binafsi.

Lugage alisema wao kama Shirika la mawasiliano wanauwezo wa kumiliki mtambo huo wa taifa kutokana na uwezo mkubwa na kazi nzuri wanayo ifanya kuwahudumia watanzania katika mawasiliano.


Waziri wa ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbarawa alisema Serikali haiwezi kuwaachia TTCL kumiliki mkonga Wa taifa kwa asilimia zote jambo linaloweza kupelekea Makampuni mengine kuja kununua Mkongo na kuuwa shirika.

Mbarawa alisema atajaribu kuongea na Serikali na Viongozi ikiwezekana serikali imiliki 30% na shirika hilo kumiliki 70% ya Mkongo wa Taifa ilikuyafanya makampuni mengine kutumia Mkongo wa Taifa na serikali kujiingizia mapato kupitia Mawasiliano.

"Kuhusiana na suala la Mkongo wa Taifa nitaongea na TCRA muweze kuingia kwenye ubia na serikali katika umiliki wa Mkongo wa Taifa naniwatake mboreshe kwanza mikongo na mitambo yenu ilitujilidhishe na huduma zenu" alisema Mbarawa.

Mbarawa alisema pia Serikali inampango wa kuboresha ubora wa internet kufikia masafa ya 800 ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuifanya shirika hilo kufanya kazi kwa uhakika zaidi.

Aidha amewaomba watumishi wote waweze kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano ilikuweza kutoa huduma zenye ufanisi na umakini wa hali ya juuu.


Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TTCL nchini Dr Kamugisha Kazaura alisema serikali inampango wa kuiboresha kampuni hiyo ilikuweza kuwarahisishia Watanzania huduma za Mawasiliano,hivyo aliwaahidi watanzania shirika hilo limejipanga ipasavyo kuhakikisha huduma hizo zinaboreshwa na Wanatanzania wanapata huduma zenye viwango vya kujitosheleza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post