RAIS MAGUFULI ATOA MCHANGO WA SHILINGI MIL 10 KWA AJILI YA KANISA HUKO CHATO




Rais Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa la bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchangia upanuzi wa kanisa hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.


Kabla ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao unaendelea.


Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao unachangiwa na waumini wenyewe.


Padre Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527