MSANII MAARUFU AFARIKI AKIIMBA JUKWAANI



Huzuni na mshangao umeghubika Indonesia baada ya muimbaji maarufu Irma Bule, aliyekuwa akiwatumbuiza mashabiki wake kuanguka na kufariki dunia jukwaani


Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata dakika 45 zilizotangulia katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Java Indonesia.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.

Japo nyoka huyo alikuwa ameng'olewa chonge zake , kwa njia moja au nyingine aliweza kum'gata na kuingiza sumu ndani ya damu yake.

Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.

Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang'amua hali haikuwa nzuri.

Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.

Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post