Mwanamume huyo aliumwa na buibui huyo akitumia choo cha kusafirishwa eneo ambalo kunafanywa ujenzi mjini Sydney.
Aliumwa na buibui aina ya redback katika uume wake. Msemaji wa hospitali ya St George Hospital alithibitisha kwamba kijana huyo alifika hospitalini na kutibiwa.
Mtu anapoumwa na buibui hupata maumivu makali, kutokwa na jasho na pia kupata kichefuchefu.
Mwanamume huyo baadaye aliruhusiwa kuondoka hospitalini na matabibu wanasema maisha yake hayamo hatarini.
Ingawa kumewahi kuripotiwa visa vya watu kufariki baada ya kuumwa na buibui aina ya redback, hakuna aliyefariki tangu kugunduliwa kwa dawa ya kumaliza sumu mwaka 1956.
Via>>BBC
Social Plugin