ACT- Wazalendo Wamteua Juma Saanani Kuwa Mrithi wa Samson Mwigamba


MAAZIMIO YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KUFUATIA KIKAO CHAKE CHA
JUMATATU TAREHE 25 APRILI 2016


Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT-Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida jana (Jumatatu) tarehe 25 Aprili 2016 Jijini Dar es Salaam.


Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu:
1. Ilimteua Ndugu Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hadi pale uchaguzi mkuu wa ndani ya chama utakapofanyika.


Uteuzi huu unafuatia kung’atuka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Samson Mwigamba anakwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.


Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Juma Saanani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar).


2.Ilipitisha Mpango Mkakati wa Chama utakaongoza programu za chama kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2020).


3.Aidha, kwa kuzingatia mamlaka yake kikatiba (Ibara ya 29 (25iv), Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe (MB) amemteua Ndugu Samson Mwigamba kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama na Kamati Kuu imekwisharidhia uteuzi huo.


Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia kuwa Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi makao makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo.


Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kuwa Umma.
Jumanne, 26 Aprili 2016.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post