RAIS MAGUFULI AWAPA SIKU 15 WAKUU WA MIKOA KUONDOA MAJINA YA WAFANYAKAZI HEWA NA WANALIPWA MSHAHARA MPAKA SASA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema jumla ya wafanyakazi 202 katika halmashauri 14 katika mikoa ya Singida na Dodoma waligundulika kuwa hewa na kulipwa mishahara kila mwezi.









Rais ameyasema hayo alipokuwa akiwakumbusha wakuu wa kikoa wapya ambao amewaapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam.





''Kwa mikoa miwili tuu wafanyakazi hao 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi''.Amesema Rais Magufuli



Kwa msingi huo kwa halmashauri 180 nchini ina maana kwa mahesabu ya haraka haraka kuna wafanyakazi 2000 na zaidi wanalipwa mishahara hewa.



Hivyo Rais Dkt Magufuli ametoa agizo kwa wakurugenzi wa taasisi za serikali kuanzia leo ndani ya siku 15 kuhakikisha wanapitia majina ya waajiriwa wote wa serikali na kuondoa majina ya ambao wanalipwa bila kufanya kazi.


==>Tazama Video hii Kumsikiliza Rais Magufuli Akiongea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527