MKE WA RAIS WA VIETNAM AKUTANA NA MKE WA RAIS WA TANZANIA,ANGALIA PICHAMke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam.Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post