MAAFISA WATATU WA JESHI LA ZIMAMOTO WASIMAMISHWA KAZI KWA WIZI WA MAFUTA YA NDEGE




Serikali imewasimamisha kazi Maafisa 3 wa Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya Ndege na mmoja kati yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.

Akizungumza katika Ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika Viwanja vya Ndege vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mhandisi Hamad Masauni amewataja walio simamishwa kazi ni Khalfani Kisana na Mussa Mandauli ambao walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya Ndege wakiwa na gari la Serikali lenye usajiri STJ 2948 huku askari mwingine aliyejulikana kwa jina la Abas Mwanza akishutumiwa kwa kosa la kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport |Lucas Maganda kwa kosa la kuiba mzigo wa abiria.


Akiwa katika kiwanja hicho Mh.Masauni amekagua utendaji kazi katika idara ya Uhamiaji,Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza viongozi wa idara hizo zilizopo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post