Heh!! AMUUA MWENZAKE KWA KISU WAKIBISHANA NANI MKALI KATI YA MESSI NA RONALDOPolisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga kisu rafikiye waliyekosana kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.

Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.

Inspekta mkuu wa polisi Kiran Kabadi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Michael Chukwuma, 21 ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai.

Yamkini yeye na mwenzake walianza gumzo kuhusu mchezaji bora katika kitongoji kimoja cha Nallasopara.Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

''Mmoja wao alikuwa ni shabiki sugu wa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Messi huku marehemu akimshabikia mfungaji mabao wa Ureno na Real Madrid Ronaldo''.

''Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.'' alisema Inspekta hyo wa Polisi.

Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika, aliongezea Kabadi.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post