HAYA NDIYO YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA SHINYANGA (RCC)


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Anne Kilango Malecela(kulia) akizungumza jana (Machi 23,2016)katika Kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kikao hicho kimehudhuriwa na mwenyekiti wa CCM,mkoa,katibu tawala wa mkoa,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri,wakurugenzi wa mamlaka wa serikali za mitaa,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya,viongozi na watendaji wa mashirika,taasisi za umma na binafsi,waandishi wa habari na wageni mbalimbali.Kikao hicho cha kamati ya ushauri ya mkoa ni kikao cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2015/16.Ni kikao cha 27 ambacho kipo kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha sheria ya tawala za mikoa namba 19 ya mwaka 1997.Hiki ni kikao cha kisheria kinachotoa ushauri utakaomsaidia mkuu wa mkoa kutoa miongozo ya maelekezo ya utakelezaji wa shughuli za serikali katika mkoa.


Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Anne Kilango Malecela alisema mkoa unaendelea na shughuli za ulinzi na usalama pamoja kusimamia maendeleo na upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.


Alisema mkoa wa Shinyanga hivi sasa unaendelea na ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa na zile za wilaya ya Kishapu na Shinyanga,ambapo alisema maandalizi ya kufungua hospitali ya wilaya ya Kishapu yapo katika hatua nzuri na atakayefungua hospitali hiyo rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Kilango alisema pia mkoa unaendelea kutekeleza mradi wa maji ya ziwa Victoria unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya wizara ya maji,mamlaka ya maji safi na maji taka ya Kahama na Shinyanga(KASHWASA),Mgodi wa almasi wa Mwadui na halmashauri ya Kishapu,ambao hadi kufikia Februari 2016 umefikia asilimia 55 ya utekelezaji.


Kilango alisema mkoa una azma ya kurejesha heshima ya mkoa wa Shinyanga kimichezo na kuhakikisha kuwa timu za Stand United na Mwadui Sports zinafanya vyema hivyo kuwataka wadau kusaidia timu hizo kkwa hali na mali.


Hata hivyo alisema hali ya upatikanaji wa chakula kwa baadhi ya maeneo kwa sasa siyo nzuri kwa sababu katika msimu wa kilimo 2014/2015 kulijitokeza ukame ulioathiri uzalishaji wa mazao ya chakula na mkoa umekuwa ukifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na hali hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakazi wa Shinyanga kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa UKIMWI kutokana na kile alichodai kuwa ushamiri wa maambukizi bado ni mkubwa katika mkoa huo.Alisema maambukizi ya UKIMWI katika mkoa wa Shinyanga ni asilimia 7.4 ukilinganisha na maambukizi ya kitaifa ambayo ni asilimia 5.1.


Alisema ni vyema jamii ikaendeleza jitihada za kuzuia maambukizi mapya kwani ugonjwa huo huathiri nguvu kazi ambayo ni muhimu katika shughuli za uzalishaji.
Katika hatua nyingine aliwataka watendaji wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi na wadau mbalimbali wa elimu kushirikiana katika kumaliza tatizo la upungufu wa madawati katika shule za mkoa wa Shinyanga.

Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipitisha ombi la kupandisha hadhi ya halmashauri ya mji wa Kahama kuwa manispaa.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Anne Kilango Malecela akizungumza

Aliyesimama ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akizungumza katika kikao hicho
Afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akitoa taarifa ya maendeleo ya sekta ya elimu katika mkoa wa Shinyanga ikiwemo suala la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza,madawati katika shule za mkoa huo na ufaulu wa wanafunzi katika mitihani mbalimbali ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2015

Wajumbe wa kikao cha ushauri wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini


Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ya Ushetu,Msalala na Shinyanga wakiwa ukumbini

Wajumbe wa kikao cha ushauri wa mkoa wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea


Kikao kinaendelea

Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini
 
Kikao kinaendelea


Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika mkoa wa Shinyanga,Simiyu na Geita ,Dr. Sekela Mwakyusa akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na shirika la Agpahi katika mkoa wa Shinyanga hususani katika eneo la huduma za VVU na UKIMWI kwa watoto chini ya miaka mitano.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'humbi akizungumza katika kikao hicho

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza katika kikao hicho,kushoto ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Anne Kilango Malecela
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post