Tuesday, March 22, 2016

CHIDI BENZ APELEKWA BAGAMOYO KUSAIDIWA AACHE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

  Malunde       Tuesday, March 22, 2016


Meneja wa Diamond, Babutale akishirikiana na Kalapina wamemchukua Chidi Benz na kumpeleka Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. 
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni rapa huyo kuomba msaada baada ya kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimkabili. 
Kupitia instagram, Babutale amepost video na kuandika:


"Mwana amekubali kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini" 
Katika video hiyo Babu Tale alisema wamefika salama Life and Hope Rehabilitation Organization, Huku Kalapina akiomba mungu kumsaidia Chidi Benz.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post