ANGALIA PICHA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU DAR LEO,WATU WENGI WAMEFARIKI DUNIA



Ajali Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam ikihusisha malori mawili na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto kuelekea Ubungo 

Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali ya Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25 wakijeruhiwa.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.



















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post