WANANCHI WA IGUNGA WAFURAHIA MRADI JUMUISHI WA AFYA YA UZAZI NA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU UNAOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA EGPAF




Mratibu wa Afya ya Uzazi, na mtoto wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora Bi. Beatrice Mushi akiongea na waandishi wa habari mkoa wa Tabora wakati wa ziara yao kutembelea mradi Jumuishi wa Afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wilayani Igunga iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mradi huu unatekelezwa na halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Kushirikiana na Shirika la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa Marekani, kupitia shirika lake la USAID. 
Mushi alisema wilaya ya Igunga ina jumla ya Vituo vya afya 55 vinavyotoa huduma hizo kupitia mradi huu. Pia amelishukuru shirika la EGPAF kupitia ufadhili wa USAID kwa kuwezesha utekelezaji wa shughuli hizo Wilayani Igunga ikiwemo kuwajengea uwezo watoa huduma wa afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vinavyowezesha utekelezaji mzuri wa huduma ya afya ya uzazi.





Afisa muuguzi Bi. Lydia Mwanga akielezea jinsi ambavyo wilaya ya Igunga imefaidika na huduma shirikishi ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa akina mama. Huduma hii pia inafadhiliwa na Shirika la USAID kupitia Shirika la EGPAF.Nyuma yake ni Mratibu wa mawasiliano na utetezi wa EGPAF bi Mercy Nyanda na Mratibu wa EGPAF wa Wilaya ya Igunga na Bw. Gervas Shibuda wakifuatilia kwa umakini maelezo hayo.
 
Mratibu wa mawasiliano na utetezi wa EGPAF, Bi Mercy Nyanda (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na kikundi cha akina mama cha Tupendane, katika kituo cha Afya cha Choma wilayani Igunga. Akina mama hao walieleza kuwa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto zinatolewa kwa ufanisi katika kituo hicho na pia zimewawezesha kupata watoto wasio na maambukizi ya VVU na kuwaacha wao wakiwa na afya nzuri.



Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dkt.Fidelis Mabula akiushukuru ushirikiano mzuri wa Shirika la EGPAF katika kutekeleza mradi wa Afya ya Uzazi katika Wilaya ya Igunga. Alisema EGPAF imefikisha huduma hizo katika maeneo yote wilayani humo na wananchi wamefaidika na huduma hizo.


Akina mama wakifurahia huduma za Kliniki ya mama na mtoto  katika Hospitali ya Igunga,ambapo wameisifu huduma hiyo na kuwaomba akina mama na baba wahakikishe wanatumia huduma za kliniki ya afya ya uzazi kikamilifu bila kukosa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527