WAHAMIAJI HARAMU 15 WAKAMATWA MKOANI SINGIDA


Wizara ya mambo ya ndani ya nchi idara ya uhamiaji mkoa wa Singida imewakamata wahamiaji haramu kumi na tano waliokuwa wakitoka nchini Ephiopia na kuelekea Afrika Kusini na kufanya jumla ya wahamiaji 30 kukamatwa mkoani Singida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Desemba mwaka Jana hadi Januari Mwaka huu. 


Akieleza afisa uhamiaji mkoa wa Singida DCI Faith Ihano amesema wahamiaji hao haramu wamekamatwa na askari wa uhamiaji wakiwa katika doria wamekutwa wamehifadhiwa katika nyumba moja eneo la unyakindi manispaa ya Singida wakisubiri kusafirishwa kwenda Afrika Kusini. 


Katika hatua nyingine DIC Ihano amesema wahamiaji hao haramu kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakisaidiwa na baadhi ya watanzania wana ofanya biashara haramu ya kuwasaidia kupita nchini kwa njia ambazo siyo za halali na atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani. 

Wahamiaji hao haramu ambao wote hawajui kuongea kiswahili wala kingereza isipo kuwa mmoja wao Bwana.Mohamed Ndermon anaye ongea Kiingereza kwa shida ,wamesema walikuwa wakienda Afrika Kusini wakitokea nchini Kenya kwa kutumia usafiri wa gari dogo kwenda kutafuta maisha. 

Kuhusiana natukio hilo idara ya uhamiajia mkoni Singida ina mshikilia mmiliki wa nyumba abayo wahamiaji hao haramu walikuwa wamehifdhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527