RAIS MAGUFULI: WENYE MALALAMIKO KUHUSU KINACHOENDELEA ZANZIBAR AENDE MAHAKAMANI



Rais Dakta.John Pombe Magufuli amesema hataingilia mgogoroo wa Zanzibar na kuwataka wenye malalamiko waende mahakamani.
Akiongea na wazeee wa mkoa wa Dar es Salaam rais Magufuli amesema katiba ya Zanzibar imeweka uhuru wa tume ya uchaguzi kama ilivyo tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kama kiongozi anayeheshimu utawala wa sheria hawezi kuingilia suala hilo. 


Dkt Magufuli ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuongea na wazee wa Dar es Salam tangu kuingia madarakani ameomba watanzania kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kudhibiti wabadhirifu ili kuelekeza fedha zitakazopatikana kwenye mipango ya maedneleo nakuapa kutovumilia wala rushwa na wazembe huku akionya wanaokejeli kuwa kasii yake ni nguvu ya soda.

Kuhusu michango rais amesema katika elimu michango yote ni hiari na kwamba wakuu wa mikoa na wilaya watapimwa kwa kadiri wanavyotekeleza wajibu wao kwa kutatua kero za wananchi ikiwemo kero ya madawati.

Rais hakuacha kusisitiza watanzania wazalendo kutumia fursa ya serikali ya awamu ya tano kuwekeza katika nchi yao kwa kadiri wanavyoweza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527