KAULI NZITO YA RAIS MAGUFULI KUHUSU ZANZIBAR :SITAINGILIA,NITAENDELEA KUKAA KIMYA,LAKINI ATAKAYELETA CHOKOCHOKO ATASHUGHULIKIWA

Feb 13 2016 Rais John Pombe Magufuli alikutana na Wazee wa Dar na kulihutubia Taifa katika ukumbi wa Diamond Jubilee, hapo hapo akachukua time yake kuyawasilisha ya moyoni. 
 Hii ndiyo kauli yake kuhusu Mgogoro wa Zanzibar 



"Kuhusu suala la Uchaguzi wa Zanzibar ,kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar,Lakini kama ilivyo kawaida kwa Tume za Uchaguzi zilizo huru duniani,Haiwezi Ikaingiliwa na rais yoyote...ZEC INA UHURU WA KUAMUA MAMBO YAKE,NA HAIWEZI KUINGILIWA NA MTU YEYOTE,Kama kuna tafsiri yoyote mbaya ,ambaye anataka kutafsiri aende mahakamani,Mahakama ipo hapo,hutaki kwenda,halafu unamwambia Magufuli Ingilia...nenda Mahakamani wakatoa tafsiri iliyo ya Haki, kwa hiyo Siingilii,Nitaendelea kukaa Kimya,Jukumu langu kama amiri jeshi mkuu ni kuhakikisha usalama wa Zanzibar,Pemba na Tanzania unaimarika...Yeyote atakayeleta chokochoko mahali popote,wajue vyombo vya sheria vipo kwa ajili ya kuwashughulikia..."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527