MBUZI NA KONDOO ZAIDI YA 70 WAUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA HUKO MOROGORO,WAZIRI AIBUKA ENEO LA TUKIO



February 9 2016 waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba alilazimika kusafiri haraka hadi mkoani Morogoro kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero, baada ya taarifa za mapigano ya wakulima na wafugaji kumfikia, safari hii yameingia kwenye headlines nyingine ya kuuwawa zaidi ya mifugo 75 kati ya mifugo 200 waliojeruhiwa kwa mapanga.




Waziri Mwigulu amefika eneo la tukio na kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza kamati ya ulinzi ya mkoa na wilaya, kufanya uchunguzi na kuwatafuta wahusika wa tukio la kukatwa katwa mapanga kwa zaidi ya mifugo 75, ili wafike mbele ya mikono ya sheria nakuagiza mahakama kupitia upya hukumu iliyotolewa mwaka 2015 ya kugawa mipaka kati ya eneo la wakulima na wafugaji.



Mwisho waziri Nchemba ameagiza uongozi wa mkoa na wilaya kufanya mkutano wa hadhara wa wakulima na wafugaji tarehe 20/02/2016, ili kuanza harakati za kumaliza mgogoro. Kati ya mifugo inayotajwa ni mbuzi, kondoo na ndama.

















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527