Majanga ya Katavi!! BABA AMUUNGUZA MOTO MTOTO WAKE BAADA YA KUKOMBA MBOGA AINA YA CHAINIZI KWA AJILI YA MLO WA MCHANAJeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda linamshikilia John Noel Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kumchoma na moto mtoto wake wa kiume aitwaye George Noel (4) viganja vyote viwili vya mikono yake.

Baba huyo amemuunguza vibaya motto wake na kumsababishia kulazwa hospitalini baada ya kumtuhumu kuwa amekomba mboga aina ya chainizi

Afisa ustawi wa jamii wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Oscar Mkenda aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hilo la unyanyasaji na ukatili lilitokea juzi katika Mtaa wa Nsemlwa .

Alisema mtoto huyo aliyechomwa moto na kuungua vibaya katika viganja vyake vya mikono yake yote miwili amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika wodi ya watoto namba 4.

Baba wa mtoto huyo ambaye anashikiliwa na polisi anadaiwa kumchoma na moto mtoto wake huyo baada ya kumtuhumu kuwa amekomba boga aina ya chanizi zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya mlo wa mchana.

Akizungumza na Malunde1 blog,Muuguzi wa wodi hiyo Joseph Mkangwa alisema hali ya mtoto huyo bado sio nzuri kutokana na majeraha makubwa ya moto aliyokuwa nayo.

Alisema bado mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu huku akiwa analelewa na bibi yake mzaa mama yake aitwaye Hadija Ally tangu alipofikishwa hospitalini hapo.

Bibi wa mtoto huyo Hadija Ally aliiambia Malunde1 blog kuwa mjukuu wake alikuwa akiishi nyumbani na baba yake mzazi baada ya mama wa mtoto huyo kuwa wameachana na mume wake mwaka jana .

Alisema inawezekana hata mke wake aliamua kuachana na kukimbia kwa mume wake kutokana na unyanyasaji kama huo walipokuwa wakiishi kama mume na mke na baada ya mke kuwa ameodoka ndipo mtoto huyo alilazimika kuishi na baba yake mzazi ambae amemtendea kitendo hicho cha kikatili na cha kusikitisha .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Mohamed Rashid na alisema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi utakapokamilika.

Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post