KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA WAKATI WA UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,POLISI WAVAMIA UKUMBI


VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuahirishwa tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani.

Jambo hilo liliwachukiza madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia.

Wakati UKAWA wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo wenyewe ,Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini,jambo lilowachukiza tena na kuibua patashika ndani ya ukumbi.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527