KANISA LACHOMWA MOTO SHINYANGA BAADA YA VIONGOZI WA KANISA KUTUMBULIWA JIPU



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange

Kanisa la True Jesus lililopo katika  kijiji cha Igalamya kata ya Usule tarafa ya Samuye wilaya ya Shinyanga limechomwa moto na watu wasiojulikana kutokana na kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya viongozi kanisa hilo walitumbuliwa jipu kwa kusimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo.
 Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange  kwa vyomba vu ahabari tukio hilo limetokea Februari 22 mwaka huu saa sita usiku.

Kamanda Nyange amesema chanzo cha tukio hilo ni baadhi ya viongozi wa kanisa hilo lililoezekwa kwa nyasi kusimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo kutokana na kuwakaribisha wageni kutoka Kenya katika kanisa hilo bila kufuata utaratibu.


Akifafanua zaidi Kamanda Nyange amesema kwa mujibu wa Askofu wa kanisa hilo Albinus Kichele viongozi waliosimamishwa kuhudumu katika kanisa hilo ni mwinjilisti wa kanisa Yona Nkuba na wainjilisti na walimu wa kanisa ambao ni John Peter,Jackson Bundala na Thereza Salamba. 
 Amesema kutokana na wageni hao kuingia bila kufuata utaratibu wa kanisa wageni hao walikamatwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga kisha kurudishwa kwao Kenya hali iliyosababisha viongozi hao wa kanisa kujitoa kwenye kanisa hilo kabla hawajasimamishwa.

Kamanda Nyangi alisema jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527