BAADA YA MAJIPU KIBAO KUTUMBULIWA KAMERA 486 ZAFUNGWA BANDARI YA DAR ES SALAAM



Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndani ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta. 
 
 
ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.
 

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini. 
 

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527