ANGALIA PICHA JINSI MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA



Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi February 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa darasani.





Mkuuwa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna




Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto.


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.


Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .


Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa 3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa darasani .




Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.



Baadhi ya wanafunzi wakiwa nje kusbiri utaratibu mara baada waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.Picha na David Nyembe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527