WABUNGE WALIANZISHA TENA- WATOKA NJE TENAHali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia hotuba ya Rais.


Baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, yalifuata matangazo na baada ya Matangazo, wabunge wakaanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli .

Wakati hayo yakiendelea, wabunge kadhaa wa UKAWA akiwemo mbunge wa Ubungo(chadema), Saed Kubeneawalikuwa wakiomba muongozo wa Naibu Spika ili waongee lakini hawakupewa nafasi.

Naibu Spika alikataa miongozo hiyo na kulitaka Bunge lijikite katika kujadili Hotuba ya Rais. Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani kwa madai kuwa wamezibwa midomo na hivyo wakaamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post