KUHUSU KIVUKO CHA MTO KILOMBERO KUZAMA KIKIWA NA ABIRIA NA MAGARI,SERIKALI YAZUNGUMZA



Serikali imesema imepokea kwa masikitiko taarifa za kuzama kwa Kivuko cha mto Kilombero na kwamba kamati za ulinzi na usalama zipo katika eneo hilo kuhakikisha hali inarejea salama katika eneo hilo.
Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama baada ya kutakiwa afanye hivyo na naibu spika wa Bunge Tulia Mwansasu kuhusiana na suala hilo.

Mheshimiwa Naibu spika serikali imepata taarifa hizo kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba watu 31 na magari na mizigo mbalimbali na kilizama jana usiku ambapo watu 30 wameokolewa huku jitihada mbalimbali zikiendelea kuleta usalama katika eneo hilo.

Aidha Waziri Mhagama amewataka wananchi kuwa makini kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa nchi itapata mvua nyingi sana pamoja na upepo mkali hivyo ni vyema wasafiri wakawa makini katika maeneo mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527