RAIS MAGUFULI AMTEUA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor of the University of Dar es salaam).

Rais Mstaafu Kikwete anachukua nafasi hiyo, iliyoachwa wazi na Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliyefariki dunia Februari, 2014.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu Jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17 Januari, 2016.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
21 Januari, 2016.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527