KUHUSU AJALI YA BASI LA BM KUUA NA KUJERUHI WATU WENGI


Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumzia ajali hiyo, amesema chanzo ni mwendo kasi na imetokea majira ya saa 3:30 usiku wa kuamkia jana ikihuhusisha basi la mwisho kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro, mali ya kampuni ya BM, baada ya dereva wake kufika Lubungo eneo lenye kona na mteremko mkali, na akiwa mwendo kasi, kukutana mbele na lori likiwa na tela, likitokea uelekeo wa Morogoro kuelekea Dar es Salaam, likiwa linamalizia kupita lori jingine lililokuwa limeegesha barabarani baàda ya kuharibika, ambapo dereva wa basi aligonga tela la lori hilo lililokuwa kwenye mwendo na kukosa uelekeo na kupindukia bondeni na kusababisha vifo na majeruhi hao.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527