Ligi Kuu soka Tanzania imeendelea uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Dar es Salaam Young Africans kuwakaribisha wagonga nyundo wa jiji la Mbeya klabu ya Mbeya City. Huu ni mchezo wa 13 kwa klabu ya Yanga ambao ndio wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi.
Yanga ambao ndio wanatajwa kuwa na kikosi bora msimu huu wa Ligi waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga klabu ya Stand United kwa jumla ya goli 4-0. December 26 Yanga wameendeleza rekodi yao ya ushindi baada ya kuiadhibu Mbeya City iliyokuwa nafasi ya 10 huku ikiwa na point 11 kwa jumla ya goli 3-0.
Licha ya kuwa klabu ya Mbeya City ilianza kwa kucheza mchezo wa kujihami zaidi kabla ya dakika ya 36 kwenda mbela kushambulia na Simon Msuva wa Yanga akaupata mpira na kutoa pasi nzuri kwa Amissi Tambwe na kupata goli la uongozi, kipindi cha mabo yalizidi kwenda mlama kwa upande wa Mbeya City baada ya Amissi Tambwe kupachika goli la pili na dakika moja baadae Thabani Kamusoko akaitimisha kwa kufunga goli la tatu.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa December 26
Mwadui FC 1-1 Simba
Ndanda FC 1 – 3 JKT Ruvu
Coastal Union 1 – 3 Stand United
Maji Maji FC 0 – 2 Prisons
Mtibwa Sugar 3 – 0 Mgambo JKT