POLISI WAKAMATA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO SIMIYU
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kukamata magunia sita ya Bangi baada ya kutelekezwa na wamiliki walipoona askari polisi waliokuwa katika doria. Akiongea na waandishi wa habari jana katika kituo kidogo cha polisi cha Lamadi wilayani Busega kamanda wa polisi mkoani Simiyu Germini Mushy amesema magunia hayo sita yenye uzito wa kilo 269 yalikamatwa kufuatia msako huo huku wamiliki wake watatu wakiyakimbia na kuacha baiskeli zao walipoona polisi.

Aidha katika tukio lingine kamanda Mushy amesema kuwa mnamo Disemba 22, mwaka huu majira ya saa 9 alasiri gari lenye namba T 366 VCJ kampuni ya J4 lilikutwa na begi likiwa na mirungi yenye uzito wa kilo 20 ndani yake.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527