Duh!! HII NAYO KALI...MSHENGA GWAJIMA AMKANA LOWASSA..ADAI HAKUWAHI KUMUUNGA MKONO LOWASSA KWENYE ILE SAFARI YA KUELEKEA IKULU


Mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima amejitokeza hadharani na kukana kwamba hakuwahi kumuunga mkono Edward Lowassa wakati wa kampeni za Urais.


Akiongea katika mahojiano maalumu na kituo cha Azam Tv, Gwajima amesema yeye hakuwahi kuwa mshirika wa Lowassa wala chama chochote, bali aliitwa jijini Arusha na Jangwani Dar es Salaam kwa ajili ya maombi tu na si vinginevyo....


Amesema kitendo cha kukubali wito huo wa maombi kimewafanya watanzania wahisi kwamba yeye alikuwa team Lowassa, kitu ambacho sio kweli.


Amedai yeye alikuwa mfuasi wa mabadiliko ya nchi, alikuwa akiunga mabadiliko ya nchi na SIO personality ya mtu au chama cha mtu.


Wakati Gwajima akikana kumuunga mkono Lowasaa, kumbukumbu zinaonyesha kuwa mchungaji huyo alikuwa ni team Lowassa na alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha mheshimiwa Lowassa anashinda kiti cha Urais.


Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Gwajima alitumia nguvu kubwa sana wakati wa kampeni kupambana na Dr Slaa ambaye wakati huo alikuwa akishusha makombora mazito kuhakikisha Lowassa hashindi huku akimtuhumu Gwajima kuwa mshenga wa Lowassa aliyemfuata kumpigia debe wampokee Chadema.


Tazama Video hii Kumsikiliza Gwajima


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527