NINAZO HAPA PICHA 10 ZA MASTAA DUNIANI ZILIZOPATA LIKES NYINGI ZAIDI INSTAGRAM MWAKA 2015

 
Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umepata watu wengi sana kwa mwaka 2015, ni mtandao ambao kila mtumiaji anao uhuru wa kupost picha na video fupi za sekunde kumi na tano…. hesabu na mimi TOP 10 ya picha zilizopata likes nyingi mwaka huu wa 2015.

10 Hiyo picha hapo juu kama unavyoiona tu ni ya Kendall Jenner ambaye ni ndugu wa Kim Kardashian ni imeshika namba 1o kwa kupata likes zaidi ya milioni 2 huku yeye akiwa na Followers zaidi ya MILIONI 45. >> Wakati ameipost hii picha ilikua anawashukuru mashabiki wake kwa kufikia idadi ya milioni 20 Instagram.9 Hiyo picha hapo juu ndio imeshika namba 9 kwa kupata followers zaidi ya milioni 2.2, ni ya mwimbaji wa muziki wa Country Taylor Swift ambaye kwa sasa ana zaidi ya followers MILIONI 60 Instagram, aliandika tu >>> ‘nimeamka hivi… na paka pembeni yangu’8 Namba 8 ndio hiyo picha hapo juu ambayo ni picha nyingine ya Taylor Swift ambayo aliweka pozi akiwa na paka.7 Namba 7 imechukuliwa na hii picha hapa juu ni ya Selena Gomez ambaye ni fashion designe, mwimbaji na mwigizaji pia na picha yake ilipata likes zaidi ya milioni 2.3, yeye mwenyewe ana followers zaidi ya MILIONI 586. Namba 6 kwenye hii Top 10 ni hii ya Taylor Swift tena ambayo ilipata likes zaidi ya milioni 2.3 akiwa na paka wake tena.5. Namba 5 ni picha ya mwimbaji Beyonce hapo juu ambaye alipozi na mtoto wake pekee aitwae Blue, ni picha ambayo ilipata likes MILIONI 2.3 kutoka kwenye fungu la followers alilonalo lenye followers zaidi ya MILIONI 55.4. Hii picha namba 4 nayo ilipata likes zaidi ya milioni 2.3, ni ya Kylie, ndugu mwingine wa Kim Kardashian, ni picha ya kuhitimu kwake Diploma, idadi ya followers wake Instagram ni zaidi ya milioni 46.3. Picha namba tatu ilipata likes zaidi ya milioni 2.5, ni ya mwimbaji wa country Taylor Swift na boyfriend wake Dj Calvin Harris.2. Taylor Swift ameitawala TOP 10, hii picha yake nyingine imepata likes nyingi ambazo ni zaidi ya MILIONI 2.6 ambayo ilikua ni picha aliyopozi pembeni ya maua ambayo alitumiwa na rapper Kanye West ambaye iliwahi kuonekana kama hawatokuja kupatana au kuongea baada ya Kanye kumnyang’anya Taylor mic kwenye tuzo alipotangazwa mshindi, Kanye alisema hiyo tuzo alistahili Beyonce na sio Taylor.

 

1. Picha namba moja ndio hii ya ndugu mwingine wa Kim Kardashian, TV Personality na Model Kendalla Jenner ambaye alipata likes zaidi ya MILIONI 3.2 akiwa na followers zaidi ya MILIONI 45.1 Instagram.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527