Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAZUIWA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA HUKO MBEYA



Wanafunzi sita wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Lupeta jijini Mbeya wameiomba serikali kuingilia kati hatma yao kielimu baada mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwazuia kufanya mtihani wao wa kidato cha nne licha ya wanafunzi hao kukamilisha taratibu zote na kupata usajili wa baraza la mitihani la taifa, NECTA.
 
Wanafunzi hao ambao wanadai kutolewa ndani ya chumba cha mtihani na mwalimu mkuu wa shule yao, wamesema wanasikitishwa kuzuiwa kufanya mtihani wao wa mwisho jambo ambalo wamedai linawaharibia maisha yao, hivyo kuiomba serikali kuingilia kati.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye baada ya kusikia uwepo wa wanahabari shuleni hapo alifunga ofisi na kuondoka huku akizima simu yake ya kiganjani.
 
Afisa mtendaji wa kata ya Iyunga, Diaz Mzee  amedai kuwa ameambiwa na mwalimu mkuu huyo kuwa wanafunzi hao walishapewa barua za kufukuzwa shule hivyo hawana sifa ya kufanya mtihani wa taifa.

Wazazi na walezi wa wanafunzi hao ambao baadhi yao ni masikini wasiojiweza wamedai kuwa uongozi wa shule haujawatendea haki watoto hao na kuomba ngazi za juu za serikali kuingilia kati kuwasaidia vijana hao kupata haki yao.
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com