Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TB JOSHUA AYEYUKA KIAINA TANZANIA...ALIKUWA MGENI WA NANI?? HAKUONEKANA WAKATI MAGUFULI AKIAPISHWA ...AACHA GUMZO

  
Mhubiri wa kimataifa nabii maarufu duniani Temipote Balogun maarufu kama TB Joshua ameacha maswali baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Magufuli.

TB Joshua aliwasili nchini November 03,2015 kwa ndege binafsi na kupokewa na Dk.MAGUFULI pamoja na Mbunge mteule Mwigulu Nchemba katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere,Dar es salaam.

Baada ya kuwasili alifanya mazungumzo ya faragha na Dk.MAGUFULI pamoja na rais mstaafu Jakaya Kikwete kisha kufanya mazungumzo zaidi ya saa tatu na Edward Lowassa.

Ujio wa nabii huyo ulionekana kama amekuja kwa ajili ya kuapishwa kwa Dk.Magufuli lakini huku baadhi ya wananchi wakifurahishwa na ujio wake na kuamini ni fursa pekee ya kukutana naye na kufanya maombi akiwa hapa nchini.

Baadhi ya watu walisema waliamua kwenda uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kumuona nabii huyo lakini haikuwa hivyo na hawakufahamu kwa nini hakuhudhuria sherehe hizo.
 
Hebu soma maoni ya Mdau huyu wa Facebook
KWA WALE WANOKUMBUKA NILISEMA JUZI KUWA NABII HUYU TB JOSHUA HAJAJA TZ KUSHEREKEA KUAPISHWA DKT MAGUFULI LAA BALI AMEBEBA UJUMBE WA MUNGU JUU YA TZ NA KANISA LAKE KITENDO CHA KUKANYAGA ARDHI YA TZ BILA VIATU NA KUKANYAGA IKULU BILA VIATU NA KWENDA KWA LOWASA AKIWA AMEVAA VIATU KINAMAANA KUBWA SANA IKOSIRI YA MUNGU YA AJABU SANA MOYO WANGU UNA TETEMEKA JUU TZ NA AKILI ZIMENIRUKA PALE AMBAPO NILITARAJIA KUMUONA JUKWAA LA WAGENI WAALIKWA UHURU STEDIUM KAMA NILIYVYO KWISHA SEMA NABII HUWA HATOKI KWENDA MAHALA POPOTE ASIPO AGIZWA NA KUTUMWA SEHEMU HIVYO SOMA 2.NYAKATI 20;20 JE WEWE NA MIMI TUMEMUONA TB JOSHUA UWANJANI KAMA TULIVYOAMINISHWA NA ITV KATIKA TAARIFA YA HABARI?
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com