Picha 24!! JESHI LA POLISI SHINYANGA LAZINDUA KAMPENI YA "ABIRIA PAZA SAUTI",ASKARI WAFURIKA STENDI YA MABASI NA KUSAFIRI NA ABIRIA




Hapa ni katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ibinzamata mjini Shinyanga.Leo Ijumaa Novemba 27,2015 saa mbili asubuhi askari wa kikosi cha usalama barabarani walitanda huku abiria na wananchi wakiwa na hamu ya kujua kulikoni!! Kumbe ni siku iliyopangwa kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni inayoitwa "Abiria Paza Sauti".


Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro amesema kampeni hiyo imeandaliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kupitia kitengp cha usalama barabarani kwa kushirikiana na kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa Mabalozi wa usalama barabarani (Road Safety Ambassadors- RSA) pamoja na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini- SUMATRA.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 24...Fuatilia hapa chini



Mabasi yaendayo mikoani yakiwa katika Stand ya Ibinzamata mjini Shinyanga leo asubuhi-Uzinduzi wa kampeni ya "Abiria Paza Sauti" umefanywa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akiwa na maafisa wa usalama barabarani kwa kutoa elimu kwa abiria wa mabasi ya masafa marefu juu ya wajibu na haki zao wanapokuwa safarini .



Mkuu wa
kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga Vicent Msame akiwatangazia abiria,madereva na wananchi wakiokuwa eneo la stendi ya Ibinzamata kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti



Maafisa hao wa polisi wakiwa na mkuu wao wa
kitengo cha usalama barabarani walipanda katika mabasi yaendayo mikoani kuanzia kituo kikuu cha mabasi Ibinzamata mpaka Tinde huku wakitoa elimu kwa abiria juu ya wajibu na haki ikiwemo kutoa taarifa wanapoona dereva yupo katika mwendo kasi ambao siyo mzuri ili kunusuru maisha yao.



Kampeni ya “Abiria Paza Sauti” ambayo ni endelevu ina lengo la kuwataka abiria kupaza sauti katika kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka ambacho huwa na abiria wengi unaosababisha madereva kuendesha kwa mwendo kasi ili kufanya safari nyingi zaidi



Mabasi yakiendelea kuingia Stand



Maafisa wa usalama barabarani wakiwa eneo la stand,wakianza kuingia kwenye basi moja baada ya jingine



Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiwa katika basi la Super Sami likitoka jijini Mwanza kwenda jijini Dar es salaam.



Maafisa wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga wakitoa muongozo kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani



Mkuu wa
kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akiwa katika basi la Kisesa akitoa elimu kwa abiria ambapo amesema kampeni hiyo wameiandaa kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa Mabalozi wa usalama barabarani (Road Safety Ambassador- RSA) pamoja na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini- SUMATRA.Kulia kwake ni mwandishi wa habari wa Azam TV Stephen Wang'anyi akiwajibika



Mkuu huyo wa
kitengo cha usalama barabarani Chacha Maro amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwataka abiria wapaze sauti kwa kutoa taarifa zinazohatarisha maisha yao wawapo safarini SUMATRA kwa kupiga simu namba 0800110019 au 0800110020 ,Trafiki makao makuu simu namba 0682887722 na kikosi cha usalama barabarani,zoezi la kutoa elimu kwa abiria litakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha abiria wanaosafiri kwa kutumia magari madogo kuepuka kuwekwa nyuma ya gari(buti) kwani ni hatari kwa maisha yao



Askari wa usalama barabarani wakijiandaa kupanda kwenye mabasi



WP Janeth Mkevela akitoa elimu kwa abiria waliokuwa wanasafiri na basi la Prince Isamilo kutoka Mwanza kwenda Moshi.Pamoja na mambo mengine aliwataka abiria kuwa jasiri kutoa taarifa wanapoona dereva anataka kuhatarisha maisha yao ,wafunge mikanda,kuhakikisha kuwa tiketi zao zina majina yao,namba za gari na siti,kufikishwa hadi mwisho wa safari yao,kudai nauli endapo chombo kitaharibika njiani na haki ya kupata huduma muhimu.




WP Janeth Mkevela akimhojia kondakta wa basi la Prince Isamilo kwanini tiketi ya abiria haina jina la abiria,namba ya gari na mahali anapokwenda



Abiria wakiwa kwenye basi wakimsikiliza afisa wa kitengo cha usalama barabarani.Abiria hao mbali na kushukuru kupewa elimu hiyo pia waliliomba jeshi la polisi kuendelea na zoezi la kupima ulevi kwa madereva ili kuhakikisha kuwa ajali zinapungua katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.



Kulia ni Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe na Malunde1 blog,bwana Marco Maduhu akiteta jambo la afisa wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Janeth Mkevela baada ya kushuka kwenye mizani ya Tinde




Baadhi ya Maafisa wa kitengo cha usalama barabarani wakiwa katika mizani ya Tinde,kila basi lilikuwa na askari mmoja



Askari wa kitengo cha usalama barabarani Mohammed Nyagal akitoa elimu kwa abiria wa basi la Zube Express juu ya wajibu na haki zao wawapo safarini



Abiria wakiwa kwenye basi,kushoto ni bwana Victor Sango ambaye ni mdau mkubwa wa Malunde1 blog akisikiliza elimu kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti



Askari wa kitengo cha usalama barabarani James Mgoha akitoa elimu kwa abiria juu ya wajibu na haki zao wawapo safarini



Abiria wakisikiliza elimu kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti.Abiria hao walitumia fursa hiyo kuzitaka mamlaka zinazohusika kudhibiti ongezeko la nauli wakati wa siku siku kuu ya Krismas na Mwaka mpya



Hapa ni katika eneo la Mizani ya Tinde-Maafisa wa kitengo cha usalama barabarani na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kurudi Shinyanga mjini baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti




Tunarudi mjini.....



Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akizungumza baada ya uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza sauti..amesema

“Tumeanzisha kampeni hii kwani katika kipindi cha mwisho wa mwaka huwa kuna abiria wengi,matokeo yake madereva wakishirikiana na wamiliki wa vyombo vya moto huendesha magari kwa mwendo kasi ili wawe na safari nyingi wapate faida hali inayosababisha kutokea kwa ajali zinazogharimu maisha ya wananchi”.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527