Makubwa Haya!! MWANAMKE AJIFANYA DAKTARI NA KUHUDUMIA WAGONJWA KISA MGANGA HAYUPO NA WAGONJWA WANATESEKA..AKAMATWA
Mwanamke mmoja mkazi wa Mwanza aliyejifanya daktari, amekamatwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, akitibu wagonjwa kinyume cha sheria. 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Redfrida Ngarapa alifika hospitalini hapo na kuingia katika moja ya chumba mganga na kuanza kuhudumia watu waliokuwa wakisubiri huduma kufuatia mganga aliyekuwa katika chumba hicho kwenda chumba cha upasuaji, ambapo hadi anakamatwa alikuwa ameshahudumia watu kumi.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kibondo Dk Kizito Luhamvya amesema walipewa taarifa na hivyo kuchukua hatua za kumkamata na kumhoji kwa kuwa hawamfahamu na si mtumishi wao.

Akizungumza wakati akihojiwa na polisi na maafisa wa hospitali hiyo, mtuhumiwa amesema alifika hospitalin hapo akiwa amempeleka mtoto wa ndugu yake aliyekuwa mgonjwa na kwamba baada ya kuona hakuna daktari akaamua kutoa huduma kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiri.

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Ruth Msafiri amesema mtuhumiwa huyo ambaye amedai kuwa ni tabibu atafikishwa mahakamani huku baadhi ya wagonjwa wakilalamikia huduma katika hospitali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post