HAYA HAPA MATOKEO YA MCHEZO WA TAIFA STARS VS ALGERIA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM






Mashabiki wa Tanzania wakati wa mapumziko walivyokuwa wanafurahia goli la Maguli

Hatimaye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Algeria Mbweha wa Jangwani ndio umechezwa leo November 14 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo wa marudiano utachezwa November 17 Algiers.

Takwimu za mchezo huo zilikuwa rafiki kwa upande wa timu zote mbili kwani kabla ya kupigwa mchezo huo, kwa takwimu za hivi karibuni Taifa Stars iliwahi kucheza na Algeria September 3 2010 Algiers na kutoka 0-0 katika mchezo wa AFCON, lakini September 3 2011 Dar Es Salaam Stars ilitoka sare ya goli 1-1 kitu ambacho kilifanya timu zote kuwa na rekodi ambazo haziwezi kumtisha mwenzake.

Licha ya kuwa Taifa Satrs ilikuwa katika nafasi za chini katika viwango vya FIFA ukilinganisha na Algeria, hiyo haikuifanya Taifa Stars ishindwe kucheza soka safi, kipindi cha kwanza Stars ilianza kwa kukosa magoli kabla ya dakika 43 Elias Maguli kupachiga goli la kwanza ambalo lilidumu kwa dakikza zote 45.

Kipindi cha pili Taifa Stars walirudi kwa kasi na Mbwana Samatta akadhihirisha ubora wake wa kupachika magoli baada ya dakika 54 kupachika goli la pili kwa Stars, furaha ya watanzania ilianza kupotea dakika ya 71 Sliman Islam alipachika goli la kwanza la Algeria na dakika mbili mbele akapachika goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Taifa Stars 2-2 Algeria.
 
Chanzo-Millardayo.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post