Duh!! KUTANA NA MGAHAWA WA AJABU..KILA KITU NDANI KINAFANANA NA SINKI LA CHOONI..WENYEWE WANAIITA " CRAZY TOILET CAFE"




Nyumba nyingi huwezi kukutana na jiko lililo karibu kabisa na choo, kwa sababu hata matumizi ya sehemu hizo mbili yako tofauti… vipi hii ya jiko na choo kwenye chumba kimoja je?




Kwenye vitu ambavyo vimenishtua leo na hii imo, yani watu wa Moscow Urusi wameona haja ya kuweka mambo tofauti… bango tu linalotangaza biashara limeandikwa Crazy Toilet Cafe, mgahawa ambao usishangae ukaagiza supu na ikaletwa ndani ya bakuli linalofanana na sinki la choo.. kuanzia kiti cha kukalia kina umbile hilo, mpaka mabakuli ya chakula na vyombo vingine viko hivyo !!


Usishtuke mtu wangu, hapo ni kiti cha mgahawa pamoja na mto wa kuegamia, alafu mambo mengine ya huduma yanaendelea.
Mgahawa wa aina hii ni wa kwanza kwa nchi za Ulaya, lakini unaambiwa hata Taiwan nako uko mgahawa ambao vitu vyake vya ndani vinafanana na sinki la chooni !!


Bango linasomeka hivyo nje ya mgahawa, Crazy Toilet Cafe

Kila mtu anakaribishwa kwa huduma poa za msosi, na bei ni ya kawaida kabisa kwa hiyo sio mahali pa kupaogopa… mfano ukafunguliwa mgahawa wa hivi Bongo utatamani kwenda na mtu wako mkaenjoy lunch?



Hii hapa video ya Mgahawa wa Crazy Toilet Cafe uliofunguliwa Moscow, Russia..

Kama hukuwahi kuijua ya mgahawa wa hivyo Taiwan nayo hii hapa mtu wangu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post