Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Pigo Tena Tanzania!! MBUNGE FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA NA ABIRIA WENGINE KWA AJALI YA CHOPA,YUMO PIA BABAAKE NA JERRY SILAAA





Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya Oktoba 15, 2015 katika Hifadhi ya Wanyama ya Selous, pembeni ya Mto Ruaha mkoani Morogoro.



Deo Filikunjombe enzi za uhai wake.




Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye alikuwa anatetea nafasi hiyo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM), amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea jana usiku ndani ya Pori la Akiba la Selous lililopo eneo la Kilombero mkoani Morogoro.



Filikunjombe ni mmoja wa abiria watatu waliokuwa ndani ya chopa hiyo ambao imethibitishwa kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jerry Silaa,Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza muda wake, Capt.William Silaa baba mzazi wa Jerry ndiye aliyekuwa rubani wa chopa hiyo ambaye naye amepoteza maisha.


“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani“— Jerry Silaa

“Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr.Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS” >>> Jerry Silaa.


Tumemtafuta Jerry Silaa lakini simu yake ilipokelewa na Msaidizi wake, Fadhili Idd ambaye amesema ni kweli wamethibitishiwa kuhusu taarifa ya Msiba na wanajiandaa na taratibu nyingine kwa sasa.


Wakati Taifa bado likiwa limeshikwa na butwaa kutokana na vifo vya aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dr Abdallah Kigoda, aliyezikwa jana na siku hiyo hiyo kutokea kifo cha Dr Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti wa NLD na mgombea ubunge jimbo la Masasi, leo tena taifa linaamka na kushuhudia kumpoteza kijana shupavu aliyekuwa miongozi mwa wabunge mahiri kuwahi kutokea ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Deo Filikunjombe.

Ni misiba..misiba..misiba, hakika uchaguzi wa mwaka huu unatengeneza historia ya aina yake na ya kuhuzunisha.

Filikunjombe anakuwa mgombea ubunge wa sita kufariki ndani ya kipindi kisichozidi majuma sita.


SOMA HAPA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA NA JUHUDI KUTAFUTA ENEO LA AJALI MBUGANI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com