Leo Jumatano Oktoba 21,2015 kumefanyika mdahalo maalum kwa wagombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mkoani Shinyanga.Mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Vijana sente Ngokolo mjini Shinyanga umeandaliwa na Radio Faraja FM Stereo kwa kushirikiana na shirika la AGAPE lengo likiwa ni kuwapa nafasi wagombea ubunge jimbo hilo kueleza kwanini wanagombea nafasi hiyo"Kwa nini wananchi wakuchague wewe kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini".
Walioshiriki ni Mgombea ubunge kupitia ACT Wazalendo Nyangaki Shilungushela,mgombea wa APPT Maendeleo Emiliana Tambwe,mgombea kupitia Chadema Patrobas Katambi aliwakilishwa na Ntobi Emmanuel wakati mgombea kupitia CCM Stephen Masele hakuonekana wala hakutuma mwakilishi.Washiriki wa mdahalo walizungumzia namna walivyojipanga kuiondoa CCM madarakani na kuboresha maisha ya watanzania,ikiwemo kuleta mabadiliko katika elimu,afya,miundombinu,kilimo,ardhi,viwanda...Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 20...kilichojiri ukumbini
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia chama cha APPT Maendeleo Emiliana Tambwe akizungumza katika mdahalo huo ambapo alieleza wazi wazi kumuunga mkono mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa huku akiomba ridhaa kuchaguliwa kuwa mbunge ili kuleta mabadiliko katika sekta ya uchumi,afya,elimu n.k
Mdahalo unaendelea
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia ACT Wazalendo Nyangaki Shilungushela akinadi sera za chama chake huku akisisitiza kuwa amedhamiria kupitia chama chake kuwaletea maendeleo wakazi wa Shinyanga
Wakazi wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Mwakilishi wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga kupitia Chadema Patrobas Katambi,Ntobi Emmanuel akinadi sera za Ukawa/Chadema ambapo alisema lengo la mgombea wake ni kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini
Wakazi wa Shinyanga mjini wakifuatilia mdahalo
Mdahalo unaendelea
Kushoto ni mtangazaji wa radio Faraja ndugu Simeo Makoba akiongoza mdahalo huku matangazo yakiruka moja kwa moja redioni,kulia kwake ni mtangazaji wa radio faraja bwana Elisha Shambiti
Mdahalo unaendelea
Wananchi wakifuatilia mdahalo
Mwakilishi wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi,bwana Ntobi Emmanuel ambaye pia anagombea udiwani kata ya Ngokolo akiomba kura kwa wakazi wa Shinyanga ili wamchague Patrobas Katambi ili awe mbunge wao
Mdahalo unaendelea
Mdahalo unaendelea
Mdahalo unaendelea
Mdahalo unaendelea
Wakazi wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Mdahalo unaendelea
Mdahalo unaendelea
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin