Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ni balaa!! ANGALIA PICHA DKT MAGUFULI AFANYA MKUTANO MKUBWA WA KIHISTORIA ZANZIBAR...AMLILIA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE ALIYEFARIKI KWA CHOPA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa visiwa vya Unguja kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana viwanja vya Mnazi Mmoja.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisisitiza kuulinda Muungano na kuwaambia kuwa atazifanyia kazi kero zilizobaki za Muungano.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Makamu wa Rais wa Dk.Gharib Bilal akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaombea kura Dk. John Pombe magufuli pamoja na Dk. Ali Mohamed Shein.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Hassan Mwinyi akihutubia kwenye mkutano wa kampeni zakuwanadi wagombea wa nafasi za urais kupitia CCM .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia wananchi na wanaCCM waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Uliofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Sheta akitoa burudani kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja.

DKT MAGUFULI AMLILIA DEO FILIKUNJOMBE


Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za vifo vya Mbunge wa Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe Ndugu Deo Filikunjombe Haule, Kepteni William Silaa pamoja na abiria wengine wawili ambao wameaga dunia Alhamisi, Oktoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta iliyotokea katika eneo la Hifadhi ya Selous mkoani Morogoro.


Katika salamu za rambirambi ambazo amewatumia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndugu Deo Sanga, na Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya Ndugu Filikunjombe na Ndugu Silaa ambavyo nimetaarifiwa kuwa vimetokea kwa ajali ya helkopta aliyokuwa akiitumia Ndugu Filikunjombe kwa Kampeni zake za Ubunge katika jimbo hilo la Ludewa.


Katika salamu zake hizo za rambirambi Dkt. Magufuli ameongeza kuwa: “Kama unavyojua, namfahamu vizuri Ndugu Filikunjombe. Alikuwa Mbunge mwenzangu katika Bunge lililomaliza muda wake mwaka huu. Nimefanya kazi naye kwa karibu na kwa miaka mitano ndani ya bunge letu.


"Alikuwa mtumishi hodari, mtumishi mwaminifu na mwadilifu kwa wananchi wa Tanzania, na hasa wananchi wa Jimbo la Ludewa, ambao aliwawakilisha kwa miaka mitano iliyopita akiwa Mbunge wao. Hata nilipofanya ziara ya kampeni katika jimbo lake la Ludewa mwezi uliopita nililala nyumbani kwake, hiyo inaonesha nilivyokuwa karibu naye. Tutakosa utumishi wake mahiri sana.”


Salamu zake za rambirambi kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Nimesikitishwa sana na taarifa ya kifo cha Baba yako Kepteni William Silaa, kwani ni tukio lisilozoeleka. Ni jana tu nimeshiriki nawe katika kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika jimbo unalogombea Ubunge, jimbo la Ukonga, naungana nawe katika kipindi hiki kigumu cha msiba mkubwa. Nakupa pole wewe binafsi, familia yenu, ndugu, jamaa na marafiki wote”.


Aidha aliongeza “Nakutumia wewe Ndugu Sanga, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Njombe salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Ndugu Filikunjombe na abiria hao wengine. Aidha, kupitia kwako namtumia rambirambi nyingi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Semamba Makinda na Wabunge wote kwa kuondokewa na mwenzao.”


Dkt. Magufuli ameongeza “Nakuomba pia unifikishe salamu zangu za rambirambi kwa wananchi wa Jimbo na Wilaya ya Ludewa ambao wamepoteza Mbunge wao aliyewatumikia kwa ustadi mkubwa kwa kipindi chote. Aliwawakilisha vizuri na kujali sana maslahi yao.

“Ametuma pia salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Ndugu Filikunjombe kwa kuondokewa na mhimili wa familia na rafiki yao mpenzi.


Amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi. "Pia naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho ya Deo Filikunjombe Haule”. Amen.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
CCM Ofisi Ndogo, Lumumba
DAR ES SALAAM.
16 Oktoba, 2015

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com