Makubwa Haya!! JAMAA WANASWA WAKISAFIRISHA POMBE HARAMU KWA KUTUMIA JENEZA....UTAFIKIRI WANA MSIBA



Tumezoea kuona majeneza yakitumika kuhifadhia miili ya Marehemu au watu waliofariki, uliwahi kufikiria kuna mtu anaweza kutumia jeneza kwa biashara zake nyingine ?!!

Stori kwenye vichwa vya habari Kenya, jamaa watano wamenaswa wakiwa kwenye mchakato wa kusafirisha pombe haramu iliyopakiwa ndani ya jeneza, safari yote njiani wameenda wakiwa wanaomboleza kama watu wanaosafirisha msiba !!



Kenya kumekuwa na stori nyingi sana mfululizo zinazohusu watu kufariki, wengine kuumwa na wengine waliwahi kuripotiwa kupata tatizo la upofu kwa sababu ya unywaji wa pombe za kienyeji.. hiyo ilifanya Serikali ipige MARUFUKU utengenezwaji wa pombe hiyo.

Stori kamili hii hapa kutoka Kituo cha KTN Television cha Kenya mtu wangu, ni video ya dakika 2:39 tu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527