MAIGE AJIGAMBA BAADA YA KUSHINDA UBUNGE MSALALA,ASEMA... KAHAMA SASA NI UTATU MTAKATIFU


Mbunge Mteule wa jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga amesema ushindi walioupata wagombea wa ccm, katika Majimbo matatu wilayani hapa ni wazi kwamba ni maendeleo ya haraka yatapatikana na kwamba ameita ni “utatu mtakatifu”.Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo Maige alisema awali maendeleo, yalishindikana kupatikana kutokana na kutokuwepo kwa ushirikiano wa kutosha baaina ya mbunge wa awali wa jimbo la Kahama, hivyo sasa anaamini kuwa sasa watashirikiana kuwaletea maendeleo wananchi.Katika hatua nyingine Maige aliwaomba wananchi wa jimbo la Kahama mjini Kuitenga siku ya Oktoba 25 kuwa wanaisherekea kila mwaka kwani ni wazi kwamba ukombozi wao umewadia baada ya kushindwa kupata maendeleo ya haraka kwa muda mrefu.“Kwanza ninafurahi sana baada ya ccm kuchukua majimbo yote matatu ya wilaya ya Kahama, Jimbo la Kahama mjini, Ushetu na Msalala, na nawashauri tu wananchi siku ya tarehe, 25 oktoba kila mwaka iwe inaazimishwa na wanakahama kama ishara ya ukombozi kwao.Kwa upande wake Mbunge mteule wa jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa, alisema baada ya kumalizika kwa uchaguzi wananchokisubiruia ni kuanza kuwatumikia wananchi baada ya kuapishwa.Aidha alisema jimbo lake lina rasilimali nyingi ambazo zitakuwa fursa kwa wananchi wake kujipatia maendeleo na hivyo kuinua uchumi wao.

Na Ndalike Sonda-Malunde1 blog Kahama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post