Hii Kali!! BAADA YA KISHIMBA KUMGHARAGAZA LEMBELI JIMBO LA KAHAMA MJINI,AMEFANYA KUFURU HII KABLA HATA YA KUAPISHWA....


Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kabla ya uchaguzi mkuu-Picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog
*********

ALIYEKUWA Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba baada ya kutangazwa kuwa mshindi ameanza kazi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia wodi ya akina mama wajawazito.

Jumanne Kishimba ndiyo yule tajiri wa Mwanza na mmiliki wa maduka ya Imalaseko,
na hii siyo mara ya kwanza kwa Kishimba kugombea nafasi hiyo,mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2000 alipogombea jimbo la Msalala.

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Kahama Mjini Anderson Msumba baada ya kumtangaza Kishimba kuwa mshindi wa jimbo hilo dhidi ya Mpinzani wake James Lembeli alianza kutatua kero za Wananchi kwa kutembelea Hospital ya Wilaya Kahama na kuwasadia akinamama wajawazito.

Msumba akitangaza matokeo hayo alisema kuwa jumala ya Wapigakura waliojiandikisha kupiga kura ni149, 304, huku waliopiga kura wakiwa 76, 280 huku wasipiga kura wakiwa 18, 280 na hivyo mshindi wa jimbo la Kahama akipata kura 47, 555.

Kishimba (CCM)aliyeshinda kwa kura 47, 555 dhidi ya Lembeli aliyekuwa Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kiasi cha kura 30,122 huku Mgombea wa ACT- Wazalendo Bobson Wambura akipata kura 605.

Akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Bruno Minja, Kishimba alisema kuwa katika kampeni zake alipata changamoto ya kero ya matatizo ya wodi ya Akinamama wajawazito kutokana na upungufu wa Vitanda pamoja na Vifaa wakati wa kujifungua.

“Niliahidi kuwa kama nitafanifanikiwa kupata ridhaa ya kuwaongoza wanakahama, nitahakikisha kuwa ninamaliza tatizo la huduma za Afya katika Hospitali ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la kujifungulia chini katika wodi ya Wazazi’’, Alisema Kishimba.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bruno Minja akitoa matatizo ya Hospitali hiyo kwa Mshindi huyo wa Ubunge wa Jimbo la Kahama alisema kuwa Hospitali hiyo imekuwa ikipkea wagonjwa wengi kutoka Wilaya mbalimbali zinazozunguka Wilaya ya Kahama.

Minja alisema kuwa katika Wodi ya Akinamama Wajawazito wamekuwa wakipokea kumla ya akinamama wanajifungua kuanzia 20- 25 huku wodi hiyo ikiwa na uwezo kupokea Wajawazito nane hali ambayo imekuwa ikisababisha kujifungulia chini.

Mshindi huyo baada ya kutembelea wodi hiyo alikuja kuongea na Wanachi na kusema kuwa masuala ya kampeni yameisha na kuongeza kuwa kama kuna watu tulikwazana wakati wa kuomba kura tusameheane na muda wa majungu umeisha hapa kazi tuu.

Mpaka kufikia hivi sasa ni matokeo ya jimbo moja tuu la Kahama Mjini ambayo yametangzwa na Mkurugnezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama yenye kata 20 huku CCM ikishinda kwa idadi ya kata 19 na CHADEMA ikipata kata moja tuu.

Wilaya ya Kahama yenye majimbo matatu ya Ubunge ambayo ni Jimbo la Msalala, ambalo Mgombea wake aliyeshinda ni Ezekiel Maige wa CCM huku Jimbo la Ushetu akishinda Elias Kwandikwa waliotangazwa na wasimamizi wa tume ya Uchaguzi.
Na Ndalike Sonda-Malunde1 blog Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527