Breaking News!! DR JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZWA RASMI KUWA MSHINDI WA KITI CHA URAIS WA TANZANIA
 
Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli(CCM) kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili wiki iliyopita.


Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr Magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,072,848 ) sawa na asilimia 39.97%Aliyeshika nafasi ya tatu ni mama Anna wa ACT aliyepata 0.65%, huku Chief Yemba wa ADC akipata 0.43%, wa tano ni Hashim Rungwe wa CHAUMMA 0.32%, huku NRA, TLP na UPDP wakipata wote asilimia 0.05.

 Dr Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee

HONGERA DK. JOHN POMBE MAGUFULI

Taarifa kamili tunakuletea hivi punde.....

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post